Wajifungulia mwembeni Ziwa Tanganyika
vilivyopo Kata ya Kipili wilayani Nkasi hawana huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na shule,
zahanati, maji na barabara.
Visiwa hivyo ni pamoja na Mandakerenge, Manda Uruira, Mavuna na Kalungu .
Gazeti hili katika uchunguzi wake lilibaini kuwa kisiwa cha Mvuna kutokana na kukosekana
kabisa kwa shule, zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wa kisiwa hicho wapatao 650 hawajui kusoma
na kuandika.
Kukosekana kwa kituo cha afya kunafanya wengi wa wajawazito kujifungulia chini ya mti
wa mwembe ambao hutumiwa kuwakusanya wananchi wakati wauguzi wanapowatembelea
kwa mwezi mara moja kutoa elimu ya afya.
Pia uchunguzi umebaini kuwa watoto wengi wa kiume waliofikia umri wa kwenda shule
wamekuwa wakikosa fursa hiyo hivyo hulazimika kuanza shughuli za uvuvi wakiwa na
umri mdogo huku wasichana wakiolewa na kuzaa katika umri mdogo baada ya kukosa fursa
hiyo ya kusoma.
Safi Kingi, mkazi kisiwani humo, amekiri kuwa hana elimu yoyote ya kutoa huduma ya afya,
anajitolea kuwasaidia akina mama pindi wanapotaka kujifungua bila kutumia vifaa vyoyote
vya kujikinga.
Alisema akisaidiana na wakunga wa jadi kuwahudumia wajawazito kisiwani humo baadaye wanalazimika kuomba au kukodi chumba kwenye nyumba yoyote ya mkazi kijijini humo.
Katika Kisiwa cha Mandakerenge ilibainika kuwa wajawazito wanalazimika kuwakodi
wakunga wa jadi kwa kuwapa Sh 10,000 ili wawasaidie kujifungua salama.
kina mama wajawazito |
Naye Mwenyekiti wa Kisiwa cha Mvuna, Clavery Kamoja alisema hali ni tete kwenye sekta
ya afya ambapo wakazi wa kisiwa hicho wanalazimika kusafiri kwa zaidi ya saa kumi kwenda kijiji Kirando ili waweze kutibiwa.
Naye, Diwani wa Kata hiyo ya Kipili , Bazilio Mbwilo amekiri kuwepo kwa kadhia hiyo visiwani humo na kuiomba Serikali kuvipatia visiwa hivyo kipaumbele katika jitihada za kutatua changamoto hizo zinazowakabili wakazi hao.
mama na mtoto |
kwa ajili ya shughuli za uvuvi pekee, hivyo hakuna uwezekano wa Serikali kujenga shule na zahanati.
“Hakuna sababu kuendelea kuwafariji wale wananchi, kutokana kukiukwa kwa sheria na
eneo lao lina mazingira magumu kutokana kusheheni mawe mengi kiasi cha kuwalazimu hata wakazi wa kisiwa hicho kujenga nyumba zao mita mbili kutoka usawa wa ziwa, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mazingira’ alisema.
No comments:
Post a Comment