Hali ya majeruhi aliyeliwa nyama za uso wake na mwajiri wake
katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko Mkoani Kigoma ijumaa iliyopita bado
tete kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata wakati wa tukio hilo
Majeruhi huyo aliyelazwa katika Hospitali ya wilaya ya
Kibondo mkoani Kigoma anakabiliwa na wakati mgumu wa kimatibabu kutokana na
matabibu kueleza kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji wa kuweka ngozi nyingine
usoni baada ya iliyokuwepo awali kuisha kabisa katika tukio hilo
Anavyoonekana sasa Kijana Susuruka |
Imeelezwa kuwa matibabu ya kijana huyo aliyekuwa akichunga
Ng’ombe kwa Bw Iman Paulo ambaye ndiye aliyemla nyama za uso wake anahitaji
kupelekwa India kwa matibabu zaidi
Lakini kulingana na hali duni ya kipato inayowasibu ndugu na
jamaa wanaomuuguza huenda hilo likashindikana
Akiwa Wodini akipata matibabu |
Kijana huyo aliyetajwa kwa jina moja la Susuruka alikumbwa
na mkasa wa kuliwa nyama za uso wake na mwajiri wake huyo Ijumaa usiku ambapo
muda mfupi baada ya watu kufika na kutoa msaada, mwajiri wake huyo Bw Paulo alimuacha
na kumkamata mbwa wake ambaye alimkaba shingo hadi kufa na kisha kunyonya damu
baada ya kula ulimi wote wa Mbwa huyo
Picha hii ni muda mfupi baada ya kuliwa |
Katika hali isiyo ya kawaida Bw Iman Paulo alipohojiwa na
Polisi alisema hajui chochote kuhusu matukio hayo
No comments:
Post a Comment