Chama cha albino nchini kimeiomba ofisi ya mwanasheria mkuu
wa serikali kukamilisha kanuni za sheria mpya ya walemavu ili ianze kutumika
kwa maslahi ya watu wenye ulemavu nchini
Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama cha
albino nchini Bw Mussa Kabimba alipozungumza kuhusu sababu za kutoanza kutumika
kwa sheria hiyo kama ilivyoelezwa awali
Kijana aliyekatwa mkono akiwa Hospitali alikokuwa akipatiwa matibabu |
Bw Kabimba amesema kuwa sheria ya walemavu ambayo ilipaswa
kuanza kutumika mwezi july mwaka huu haijaanza kufanya kazi kutokana na
kutokamilika kwa kanuni za sheria hiyo, kazi inayofanywa na ofisi ya
mwanasheria mkuu wa serikali
Diwani wa viti maalum (CCM) mjini Tabora Blandina Joseph |
Amesema endapo sheria hiyo itakamilika na kuanza kutumika
itasaidia kutetea haki za watu wenye ulemavu nchini na hatimaye kuimarisha
utawala bora kwa wananchi wote
No comments:
Post a Comment