Wataalam wa
mabomu kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ wamefika katika eneo la
Ruganzo wilayani Ngara
Mkoani Kagera ambako kitu kisichofahamika kimeanguka tangu jumatano usiku na kubaini kuwa kitu
hicho sio bomu
Mnadhimu mkuu wa mafunzo na utendaji kivita kutoka Briged ya
Faru Tabora Kanal Simon Hongoa amesema kuwa kitu hicho kilichoibua hofu kwa
wakazi wa eneo hilo na wilaya ya Ngara kwa ujumla sio Bomu bali ni kipande cha
Satellite kilichoanguka kutoka angani
Aidha wamekichukua kipande hicho
cha Satellite na kukihifadhi katika kambi ya jeshi la Wananchi iliyopo eneo la
K-9 wilayani Ngara
Awali kamanda wa polisi mkoa wa
Kagera Bw Philip Kalangi alisema kuwa askari waliofika eneo
hilo hapo juzi walishindwa kukitambua kitu hicho na kutoa taarifa makao makuu
ya jeshi hilo jijini Dar Es Salaam
Kipande hicho cha Satellite chenye
urefu wa zaidi ya sentimeta 50, kikiwa na umbo la yai pamoja na nyuzinyuzi
kilianguka usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo
No comments:
Post a Comment