Kijana aliyetajwa kwa jina moja la
Susuruka amejeruhiwa kwa kuliwa nyama za sehemu ya uso wake na mwajiri wake
aliyekuwa akimfanyia kazi ya kuchunga ng’ombe katika kijiji cha Muhange
wilayani Kakonko mkoani Kigoma
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Saimon
Anthony amesema kuwa tukio hilo limetokea jana usiku ambapo aliyefanya unyama
huo ni Bw Imani Paulo
Amesema kabla ya kumla nyama za usoni
mfanyakazi wake, Bw Paulo alimuua mbwa wake na kisha kula ulimi wa mbwa huyo
Kijana Susuruka anavyoonekana baada ya kujeruhiwa usoni |
Jeshi la polisi wilayani Kakonko
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo amekamatwa
ambapo baada ya kuhojiwa amesema hajui chochote kuhusu matukio hayo
Taarifa zinasema kuwa majeruhi huyo amepelekwa
katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa ajili ya matibabu
No comments:
Post a Comment