FLASH

Monday, June 18, 2012

Shivji: Kutoijua katiba iliyopo kusiwafunge midomo  

Profesa Issa Shivji

TANZANIA hivi sasa inapita katika mchakato wa ukusanyaji wa maoni juu ya katiba mpya baada ya ile ya mwaka 1977 ambayo iliundwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa wakati huo.Mchakato huo unakuja huku kukiwa na maoni tofauti juu ya mfumo wa kukusanya maoni pia kuna watu ambao wanadai kuwa hawataweza kutoa maoni kwani hawaijui katika iliyopo.
Hata hivyo, Profesa Issa Shivji wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, anapingana na dhana kuwa ili uweze kuchangia vizuri katiba basi lazima uijue iliyopo.
Anasema hoja hiyo haina mashiko na imekuwa ikitumiwa na watawala kuwafumba midomo wananchi kutoa maoni yao na wao kujifanyia wanavyotaka.
Profesa Shivji anasema hoja ya msingi ni je, katiba ya sasa ni muafaka juu ya mifumo iliyopo? Na anasema mtu si lazima awe msomi ili kuweza kujua kuwa mifumo iliyopo katika katiba haifai.
Anasema mathalani mtu anaposhindwa kumpeleka mtoto wake shule, wananchi wanapolalamikia ukosefu wa barabara ni wazi mfumo uliopo hauna msaada kwao.
"Ukusanyaji wa maoni hautegemewi kuwa mwananchi wa kawaida eti atasema Ibara namba fulani siipendi, hakuna kitu kama hicho" anasema.
Profesa huyo anabainisha kuwa ni wajibu wa wasomi kufanya uchambuzi, iwapo mwananchi anasema hana barabara anamainisha nini.
Shivji anasema ili kupata katiba kwa amani ni lazima yawepo majadiliano huru na ya wazi katika kila eneo kuanzia katika migahawa, maofisini, mitaani na kwingineko.
Anasema mijadala ndio ambayo itazaa muafaka wa katiba kwani kupitia majadiliano watu watatoa maduku duku yao, kero zao, matumaini yao na changamoto ambazo zinawakabili.
Profesa Shivji anasema ili wananchi waweze kuchangia kwa upana katiba mpya ni vizuri wakajua historia ya katiba iliyopo, kuanzishwa kwake na dhana ya katiba kwa ujumla wake.
Shivji anawaonya wananchi kuwa makini na vyama ambavyo vinadai kuwa vinatetea maslahi ya wanyonge na kusema kuwa vinaweza vikawa na migongano ya kimaslahi baina yao.
MAANA YA KATIBA
Profesa Shivji anasema nenno katiba lina tafsiri tofauti kulingana na kulingana na uelewa wa watu kwani wanasheria wanaamini kuwa katiba ni sheria mama au ya msingi ambayo inabeba zingine zote.
"Wanamainisha kuwa sheria zote zinazotungwa ni kwa mujibu wa katiba na vyombo vya utungaji wa sheria hizo pia vimewekwa kwa mujibu wa katiba" anasema.
Anasema wanasheria bobezi wamekuwa wakidai kuwa katiba ni kanuni za kisheria zilizokusanywwa katika nyaraka mahsusi zinazohusu mhimili mitatu na haki za binadamu.
Msomi wa sayansi ya siasa anasema Shivji kuwa atasema katiba ni mkataba wa kijamii baina ya watawala na watawaliwa.
Dhana hiyo ya katiba mkataba anasema inatokana na wanafalsafa wa Uingereza John Louis na Thomas Hopes miaka ya mwanzoni ya 1900.
Anasema wakati ule mfumo ambao ulianza kuenezwa ulikuwa wa kibepari ambao ulijikita katika bidhaa (ununuzi na uuzaji) hivyo dhana ya mkataba ikawa inatawala.
Mwanafalsafa anasema kuwa walitumia dhana hiyo ya mkataba kueleza katiba na hata wasomi wa sasa wakiulizwa watawala na watawaliwa walitoka wapi ili kufunga mkataba wakati ule hawatakuwa na jibu.
Anasema, wasomi wa siasa uchumi wanaamini kuwa katiba ni muafaka wa wananchi kuhusu misingi na mfumo wao wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
"Maana zote tatu za katiba zina ukweli katika maana zote tatu lakini sio ukweli kamili kwa sababu ni kama hadithi ya vipofu na wasifu wa tembo" anasema.
Profesa huyo anasema kila mmoja alimuelezea tembo anavyomjua kulingana na pale alipomshika mnyama huyo hivyo kufanya asiwepo ambaye ana wasifu kamili wa mnyama huyo.
DHANA YA KATIBA
Anasema Shivji kuwa ili kuelewe katiba ni lazima dhana yake ikaeleweka na ni vigumu kuelewa dhana ya katiba bila kuangalia historia
"Kwangu mimi dhana ya katiba inatokana na historia ya nchi za Ulaya na ni lazima kukiri kuwa itikadi na hata dini zetu zinatokana na nchi hizo" anasema.
Anabainisha kuwa wazungu ndio ambao walitawala ulimwengu katika karne ya 15 na hadi leo hii labda bado dhana nyingi zinatokana na wao ikiwa ni pamoja na masuala ya elimu.
Historia ya dhana ya katiba anasema ilizaliwa wakati wa mchakato wa mageuzi na mapinduzi ya kutoka katika mfumo wa ukabaila kwenda wa kibepari.
Anafaafanua kuwa mfumo wa ukabaila msingi ambao ulikuwa unawajumuisha mabwana na watwana ambao ulifanya mkuu wa mamlaka kuwa mfalme.
"Chini yake walikuwepo mamwinyi ambao walikuwa wamehodhi umiliki wa ardhi" anasema na kuongeza kuwa mfumo huo ulihalalishwa na itikadi za dini.
"Kuubadili mfumo watawala wakati huo wakaleta utawala waliouita wa sheria ambao msingi wake ni ubepari" anasema na kwa kutumia misingi hiyo ndipo ilipozaliwa dhana ya katiba.
"Turidhia dhana hiyo kwa sababu tulitawaliwa na nchi za magharibi" anasema hata katiba mbili zilizopata kuandikwa kabla na baada ya uhuru zinaegemea huko.
Shivji anasema mapambano ndio ambayo yalizaa dhana ya katiba na suala hilo likiwekwa katika nadharia anasema kuwa katiba kama sheria ni uwanja wa mapambano.
"Wahenga wanasema sheria ni msumeno maana yake shheria ni uwanja wa mapambano ni vizuri sana kina mwanananchi akaelewa hilo" anasema.
Profesa Shivji anaongeza kuwa anaposema hivyo anamainisha kuwa kuna mgongano wa kimaslahi baina ya wanajamii kutokana na Taifa kugawanyika kimatabaka hivi sasa.
Anasema mgongano ni lazima kutokana na jamii kugawanyika katika makundi tofauti na njia pekee ya kupata muafaka wa katiba kwa njia ya amani ni majadiliano.
Anasema upande mmoja wa makundi hayo wapo watawala wa kiuuchumi kwao katiba ni chombo cha kuhalalisha utawala wao ili udumu na mfumo wa uchumi wanaosimamia usisambaratike.
"Hivyo kama wana mgongano ni wazi kuwa Taifa linaweza kusambaratika ndio maana wanaotawala muhimu kwao ni kuhalalisha utawala wao na ule kiuchumi ili ukubalike na watawaliwa.
Upande mwingine watawaliwa ambao ni wengi katiba ni fursa kwao ya kuweka mipaka na madaraka ya watawala ili angalu wasikandamizwe na haki zao zisibanwe.
Pia kundi hilo linataka maslahi yao angalau yatambuliwe katika katiba
Anasema Shivji kuwa ni vigumu kuangalia dhana ya katiba bila kuangalia muktadha huo wa mapambano lakini la msingi ni kuwa lazima uwepo muafaka.
"Huo muafaka baada ya mgongano ndio ambao utaingia katika katiba na ni wa kiasi gani itategemea nguvu za mvutano wa matabaka"anasema.
itaendelea.........

No comments:

Post a Comment