Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Kaptein Honest Erenest Mwanossa amesema baadhi ya miradi ya Serikali imekuwa ikitekelezwa chini ya kiwango tofauti na miradi ya watu binafsi kutokana na ubinafsi wa baadhi ya watumishi
|
Mkuu wa wilaya ya Ngara Constantine Kanyasu akiupokea Mwenge kwa Mkuu wa wilaya ya Karagwe |
Kaptein Mwanossa ametoa kauli hiyo Hivi Karibuni alipokuwa akizindua Bwalo katika shule ya Sekondari ya RHEC iliyoko Rulenge wilayani Ngara Mkoani Kagera
|
Kaptein Mwanossa akiongoza wimbo ulioambatana na zoezi kuwachangamsha maafisa mbalimbali |
Amesema kukosekana kwa uzalendo miongoni mwa watumishi wa serikali wanaopewa jukumu la kusimamia miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa majengo mbalimbali kunasababisha wengi wao kutaka kujinufaisha na kuiibia serikali hali inayosababisha majengo kujengwa chini ya kiwango pamoja na thamani ya ujenzi kutowiana na jengo husika
|
Mkuu wa wilaya ya Ngara Constantine Kanyasu akimkabidhi Kapt Mwanossa risala ya Utii kwa rais wakati wa mbio za mwenge wilayani Ngara |
Kapt Mwanossa amesema jengo la Bwalo hilo la RHEC sekondari linawiana na thamani yake ya shilingi milioni 90 kwa kuwa limesimamiwa vizuri na hasa kwa kuwa ni la mtu binafsi
Aidha amesema miradi ya maendeleo inapojengwa inafaa kuwanufaisha wananchi wa maeneo husika kwa kuhakikisha baadhi ya vitu kama kokoto na mchaanga vikusanywe na wananchi ili kuongeza vipato vyao
|
Kapt. Mwanossa akizungumza jambo |
Pia amemtaka mkuu huyo wa wilaya ahakikishe anasimamia kwa ukaribu miradi inayojengwa wilayani kwake ili iwe na ubora unaostahili pia ikamilike kwa wakati
No comments:
Post a Comment