FLASH

Saturday, September 1, 2012

SITTA; WIMBI LA WAHAMIAJI HARAMU NCHINI NI MATUNDA YA UZEMBE WA VIONGOZI NA WANANCHI WA MIPAKANI



Waziri wa Jumuiya ya afrika mashariki Bw Samwel Sitta amewataka viongozi na wananchi wa maeneo ya mipakani kuzidisha umakini kuhusu watu wanaoingia nchini kutoka mataifa mbalimbali ili kukabiliana na ongezeko la wahamiaji haramu

Waziri Sitta ametoa wito huo alhamisi wiki hii wakati akizungumza na watumishi wa idara mbalimbali za serikali walioko katika mpaka wa Kabanga wilayani Ngara mkoani kagera wakati wa ziara yake wilayani Ngara

Bw Sitta amesema kuwa viongozi na wananchi wa mipakani wamekuwa wakirahisisha uingiaji wa wageni nchini na kutotoa taarifa ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria
Waziri Sitta (Kulia) akiwa na mkuu wa wilaya ya ngara Constantine Kanyasu
Aidha Bw Sitta amesema kuwa shilingi milioni 400 zilizotengwa na serikali kwa ajili ya kuwarudisha makwao wahamiaji 18000 waliodhihirika zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo badala ya kuwarejesha kwao wahamiaji hao waliongia nchini kutokana na kutokuwa makini kwa viongozi na wananchi wa mipakani
Waziri Sitta akiwasalimia watumishi wa mpaka wa Kabanga kati ya Tanzania na Burundi
Awali mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine kanyasu alimwambia waziri Sitta kuwa idadi kubwa ya wahamiaji haramu ni moja ya changamoto zinazoikabili wilaya ya Ngara
Samwel Sitta wa pili kulia akiwa na DC Ngara,RPC Kagera Philip Kallangi na M/kiti CCM wilaya ya Ngara
Waziri huyo pia akakiri kutelekezwa kwa mipaka ya Tanzania nan chi nyingine kutokana na changamoto zinazoainishwa kila siku na watumishi wa idara mbalimbali zilizoko mipakani ikiwemo pia wimbi la wahamiaji haramu
Waziri Sitta akisalimiana na watumishi kabla ya kuingia ukumbini katika mpaka wa Kabanga
Katika hatua nyingine waziri huyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amewataka watanzania kutunza vizuri chakula ili kukabiliana na baa la njaa litakaloyakumba mataifa mbalimbali duniani hapo mwakani

Bw Sitta amesema kuwa mwaka 2013 utakuwa na njaa kali katika mataifa mbalimbali duniani kutokana na ukame ulioikumba Marekani ambao ndio wazalishaji wakubwa wa mahindi yanayouzwa kwa nchi zenye mahitaji
Watumishi wa idara za serikali walioko mpaka wa Kabanga wakimsikiliza waziri Sitta kwa makini
Bw Sitta amesema kuwa ukame huo pia umeyakumba mataifa mengine yanayozalisha nafaka kwa wingi duniani ikiwemo Canada na kwamba hali hiyo itasababisha nchi hizo kutunza nafaka hizo kwa ajili ya matumizi yao

No comments:

Post a Comment