FLASH

Thursday, October 25, 2012

MAWAKILI KATIKA KESI YA KIONGOZI WA UAMSHO WAMEJITOA KATIKA KESI HIYO



Mawakili wa Kiongozi wa Kundi la Uamsho la Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed leo wamejitoa katika kesi hiyo kwa madai kuwa wateja wao wanafanyiwa usumbufukwa kuhangaishwa 

Mawakili hao Bw Salim Tawfik na mwenzake Abdallah Juma wametanga kujito katika kesi hiyo hivi Leo walipozungumza na waandishi wa habari huko Zanzibar muda mfupi kabla ya wateja wao Sheikh Farid na wenzake Sita kufikishwa mahakamani
Mawakili wa Sheikh Farid na wenzake sita ambao leo wamejitoa kusikiliza kesi hiyo
Uamuzi huo wameutangaza nje ya mahakama na kudai kuwa wateja wao wamekuwa wakisumbuliwa na kutopelekwa mahakamani ambapo wakati mwingine wamekuwa wakipelekwa ni Kwerekwe na wakati mwingine Vuga

Aidha baada ya kutangaza kujitoa katika kesi hiyo mawakili hao waliondoka katika viunga vya mahakama  ambapo muda mfupi baadaye wateja wao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake sita walifikishwa mahakamani wakiwa wamenyolewa ndevu zote
Sheikh Farid na wenzake sita wakifikishwa Mahakamani wakiwa hawana ndevu
Sheikh Farid na wenzake wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uchochezi hali iliyosababisha mtafaruku visiwani Zanzibar

Aidha wamepandishwa mahakamani huku wakiwa hawana Wakili baada ya mawakili wao kujitoa

No comments:

Post a Comment