Klabu ya soka ya Simba
yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi imetangaza kuwapa adhabu wachezaji wake wawili ambao ni Haruna Moshi "Boban" na Juma
Said Nyoso.
Harouna Moshi Boban kushoto na kulia ni Juma Said Nyosso |
Boban amesimamishwa kwa muda wa siku
21 kutokana na utovu wa nidhamu na kutokuwa na heshima kwa muajiri wake
(Simba) na amepewa siku 21 atoe maelezo ya kutosha
Katika wakati huo wote atakuwa
akipokea mshahara nusu bila marupurupu ya kawaida.
Kwa upande wa Juma
Nyoso ameshushwa hadi Simba B kutokana na makosa
mengi ya kiuchezaji yanayoigharimu timu yake na atarudishwa kikosi cha kwanza
pale benchi la ufundi litakaporidhishwa na kiwango chake.
Katika wakati huo
wote Nyosso atakuwa akilipwa mshahara wake kama kawaida na malipo wanayopata
wachezaji wa kikosi B.
No comments:
Post a Comment