SIMBA YAIFUNIKA YANGA KATIKA UWAKILISHI KWENYE TIMU YA TAIFA
Kocha Mkuu mpya wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, leo ametangaza Kikosi cha Wachezaji 25 kwa ajili ya Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya Makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa mjini Abidjan Juni 2 mwaka huu
Katika mechi hizo za Mchujo, Tanzania ipo Kundi C pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gambia.
Kwa mujibu wa Taarifa ya TFF iliyosambazwa na Ofisa Habari wake, Boniface Wambura, Kim amesema Timu hiyo itaingia Kambini Jumatano Mei 16 na uteuzi wake umefuata uwezo wa Mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ni Wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), George Kavishe (katikati) Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodigar Tenga na Kulia ni Kocha Mpya wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen.
Wachezaji walioteuliwa:
Makipa: Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar)
Mabeki: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo: Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji: Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).
Kabla ya kuwavaa Ivory Coast katika mechi hiyo ya mchujo, Taifa Stars, itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 dhidi ya Malawi kwa ajili ya kujipima ubavu.
No comments:
Post a Comment