Mashindano ya vijana walio na umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Kopa Coca Cola yameanza rasmi hii leo kwa mkoa wa Kagera
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Soka wilayani Ngara, Mkoani Kagera NDFA Seif Omary maarufu kama “UPUPU” amesema kuwa Mashindano hayo yanafanyika kimkoa wilayani Muleba na kushirikisha wilaya zote za mkoa huo kimichezo
Makamu mwenyekiti NDFA Seif Omary Upupu
Amesema Michuano hiyo imeanza leo kwa michezo miwili ya ufunguzi ambapo katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi rasmi umewakutanisha wenyeji timu ya wilaya ya Muleba dhidi ya wilaya ya Bukoba Manispaa
Katika mchezo huo wenyeji Muleba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watoto wa mjini timu ya wilaya ya Bukoba mjini
Mchezo wa pili uliochezwa majira ya mchana umezikutanisha timu ya Wilaya ya Ngara na Timu ya wilaya ya Misenyi ambapo timu ya wilaya ya Ngara imeibuka na ushindi wa magoli 2-1
Ushindi huo kwa timu ya wilaya ya Ngara umetoa dira kwa kikosi hicho kilicho na wachezaji 15
UPUPU amesema kuwa katibu wa NDFA Jonah Katanga ambaye ameambatana na timu huko muleba, ameeleza kuwa mchezo huo ulikuwa wa kuvutia kwa timu zote mbili ambapo Ngara ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufungwa goli hilo moja mapema kipindi cha kwanza
Amesema utulivu wa wachezaji uliifanya timu hiyo kuingia uwanjani katika kipindi cha pili ikiwa na ari zaidi na hivyo kufanikiwa kusawazisha goli hilo na kuongeza goli la ushindi
Makamu Mwenyekiti NDFA "Upupu"
Wachezaji walioko na timu ya wilaya ya ngara katika mashindano hayo ni Nelson Amon, Omary Paulo, Issa Ahmed, Erick Sylvester, Imani Anthony, Edson Emmanuel, Tumaini Anthony na Tryphone Oscar
Wengine ni Mahmoud Mussa, David Hezron, Asifiwe Buzaire, Jared Mivuba, Wisman Jackson, Jonas Rukiliza pamoja na mlinda mlango mahiri Said Ramadhan ambaye hakuweza kuongozana na timu hiyo wakati ikiondoka hapo jana kutokana na kukabiliwa na mtihani wa Mock wa kidato cha nne ambao amemalizia hii leo na kwamba muda wowote huenda akaungana na wenzake katika kuhakikisha timu hiyo inarejea na ubingwa
Viongozi wengine walioongozana na timu hiyo ni Mwalimu Teonest Venance wa Kabanga Secondary pamoja na mwalimu Deogratius Malingumu kutoka Shunga secondary
No comments:
Post a Comment