Rais Paul Kagame wa Rwanda amezishutumu nchi za magharibi pamoja na mashirika ya kimataifa na kusema kuwa ndiyo sababu ya mgogoro unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
Rais Kagame ametoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa chuo cha jeshi cha Nyakinama kilichopo katika wilaya ya Musanze
Rais Kagame katikati akiwa na maofisa wa jeshi katika ufunguzi wa chuo hicho |
Amesema kuwa Rwanda na DRC zilikuwa zikielekea kutatua mgogoro huo katika eneo mashariki mwa DRC ambako makundi yenye silaha yanaendesha harakati zake na kwamba mataifa ya magharibi yanarudisha nyuma jitihada hizo
Miongoni mwa makundi yanayoendesha harakati zao katika eneo hilo ni pamoja na Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) linalotuhumiwa kwa mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994
Kagame katika picha ya pamoja na maofisa wa jeshi baada ya ufunguzi wa Chuo hicho cha jeshi |
Aidha wakati akifungua chuo hicho rais Kagame ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuhakikisha vinadhibiti matukio kabla ya kutokea ili kuepuka athari zitokanazo na matukio husika
No comments:
Post a Comment