Polisi mjini KwaZulu Natal, Afrika kusini inamshikilia mtu anayedaiwa kumteka msichana mwenye umri wa miaka 15 na kumbaka kwa miezi mitatu mfululizo
Msemaji wa polisi nchini Afrika kusini Kanal Vincent Mdunge amesema mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kufikishwa mahakama kesho ili kujibu tuhuma za kuteka na ubakaji
Msichana huyo mkazi wa Madadeni mjini Newcastle, alitekwa Machi 29 mwaka huu na kupelekwa Chesterville mjini Durban ambako alipewa dawa za kulevya na kubakwa kila siku
Msichana huyo alifanikiwa kutoroka baada ya walinzi waliokuwa wakimlinda kupitiwa na usingizi na kwamba kwa sasa yuko katika kituo cha ushauri nasaha akijengwa upya kisaikolojia
Asanteni sana sisipamojablogspot.com kutuhabarisha
ReplyDelete