Waziri wa zamani wa umwagiliaji wa Misri Bw Hesham Mohamed Qandil ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa taifa hilo
Rais wa Misri Mohamed Morsi, amemteua Qandil na kumpa kazi ya kuunda baraza la mawaziri, ambalo Qandil mwenyewe amesema ataikamilisha kazi hiyo siku si nyingi kwa kushirikiana na Rais
Rais wa Misri Mohamed Morsi, kushoto na Waziri mkuu mteule Hesham Qandil |
Uteuzi wa leo umekuja ikiwa ni siku 25 baada ya Morsi kuapishwa kuwa Rais wa Misri baada ya Hosni Mubarak kuondolewa madarakani kwa vuguvugu la nguvu ya Umma
Qandil alikuwa waziri wa umwagiliaji katika serikali ya waziri mkuu aliyepita Kamal Ganzuri
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Qandil amesema kipaumbele chake ni kuhakikisha anaitekeleza mipango ya Rais Morsi ndani ya siku 100 inayolenga katika masuala makuu matano: ulinzi, trafiki, usafi wa umma pamoja na masuala ya mafuta
No comments:
Post a Comment