Radio ya Upinzani nchini Madagascar, Free FM imesitisha kurusha matangazo yake kutokana na vitisho kutoka Jeshi la serikali nchini humo, vilivyotolewa baada ya kutokea uasi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Meneja wa Kituo hicho cha Radio Free FM, Bw Lalatiana Rakotondrazafy, amesema matangazo hayatarushwa mpaka hapo uongozi wa kituo hicho utakapokuwa na uhakika kuwa hawatapokea vitisho vingine vya jeshi.
Lalatiana amesema kwanza waliona askari wakiingia kituoni hapo asubuhi siku ya Jumapili, wakati ambapo uasi ndio ulikuwa ukianza katika kituo kimoja cha kijeshi, jirani na uwanja mkuu wa ndege wa taifa hilo.
Amesema kwa mshangao wa watangazaji studioni hapo, askari hao walikata umeme, na kukatisha mawimbi ya matangazo hayo kwa zaidi ya saa saba mfululizo.
Meneja huyo wa radio amesema baada ya hapo askari hao walikusanyika mtaani mbele ya jengo la kituo hicho ambapo yeye (Lalatiana) kama meneja aliwaambia watangazaji na wafanyakazi wengine kukusanya vyombo vyao vya kazi na kuondoka.
Wakati hayo yakiendelea, askari hao waliwanyangánya waandishi kompyuta na kifaa cha kurekebishia umeme yaani - voltage regulator.
Wakati wa uasi huo, Free FM ilitangaza sakata hilo na kurusha hewani sauti ya askari mmoja akikiri kwamba kuna mapinduzi yanaendelea Madagascar, taarifa iliyokemewa vikali na Wizara ya Mawasiliano ikidai kuwa itakichukulia chombo hicho hatua za kisheria.
Wakati huo huo Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo ndio mpatanishi mkuu wa mgogoro wa Madagascar, inawakutanisha mahasimu hao wawili ana kwa ana hivi leo (25.07.2012).
Baadhi ya vijana wakiandamana nchini Madagascar |
SADC imewapa muda Ravalomanana na Rajoelina mpaka tarehe 31, mwezi huu kuhakikisha wanamaliza tofauti zao.
No comments:
Post a Comment