FLASH

Thursday, July 26, 2012

KANAL RUGIGANA NGABO WA RWANDA AHUKUMIWA KWA KUHATARISHA USALAMA NCHINI RWANDA


Mahakama kuu ya kijeshi ya Rwanda imemuhukumu kifungo cha miaka tisa gerezani Luteni Kanali Rugigana Ngabo baada ya kukutwa na hatia ya kuhatarisha usalama nchini humo

Jaji wa mahakama hiyo Bernard Hategekimana, amesema mshitakiwa huyo amekutwa na hatia ya kuhatarisha usalama na kuchochea vurugu na kwamba mahakama haijamkuta na hatia katika shitaka la tatu la uhaini 
Lt.Col. Rugigana Ngabo (Kulia) akiwa na mwanasheria wake Geofrey Gatare mahakamani jana
Kanali Rugigana ambaye ni mkuu wa zamani wa Kikosi Uhandisi katika jeshi la Rwanda alikamatwa mwezi Agosti mwaka 2010 na kwamba kutokana na kukutwa na hatia ya kuchochea vurugu amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela pamoja na faini ya faranga laki mbili

Hata hivyo jaji Hategekimana amesema kanal Rugigana anawezeza kukata rufaa ndani ya siku 30 ambapo tayari mwanasheria wa Rugigana amesema hawajaridhishwa na maamuzi hayo hivyo watakata rufaa

No comments:

Post a Comment