Wachimbaji saba wa makaa ya mawe wamefariki kutokana na mlipuko wa gesi kwenye mgodi wa makaa ya mawe kaskazini mwa Mexico
Mkuu wa jeshi la ulinzi kaskazini mwa Mexico Bw Francisco Contreras Obregon amesema kuwa wachimbaji hao wenye umri kati ya miaka 20 na 39, wamefariki jana baada ya mwamba kuanguka
Amesema kuwa miili yote ya wachimbaji hao waliofariki imetambuliwa na kwamba wote wametolewa katika kifusi ardhini walimokuwa wamenasa baada ya mlipuko huo
Waombolezaji wakiwa katika eneo la tukiowalipofia wachimbaji hao |
Afisa wa huduma za dharura katika serikali ya Mexico Juan Antonio Ibarra amesema kuwa miili hiyo yote imetolewa chini ya ardhi baada ya muda mrefu kutokana na migodi mingi ya makaa ya mawe kutokuwa na miundombinu ya kiusalama inayostahili
Aidha mgodi huo unadaiwa kukaguliwa mara 16 tangu mwaka 2009 na kwamba mapema mwezi june mwaka huu wakaguzi walibaini kuwa mgodi huo hauna njia ya dharura ya kutokea inapotokea tatizo
Mwaka 2006 wachimbaji 65 walikufa katika mlipuko uliotokea katika mgodi mwingine wa makaa ya mawe wa Coahuila nchini Mexico
No comments:
Post a Comment