Maafisa watatu katika Ofisi ya Waziri mkuu nchini Uganda wamekamatwa na kuwekwa kizuizini kufuatia kurugenzi ya kuchunguza ubadhirifu wa mali za umma wakidaiwa kughushi nyaraka na kusema uongo
Watuhumiwa hao waliokamatwa jana ni pamoja na mhasibu, Bw Arthur Mumanyire na makeshia wawili Bw Isiah Ounyo na Musiiho Byekwaso, wanaodhaniwa kuwa na taarifa muhimu zinazoweza kusaidia upelelezi kuhusu suala hilo
Maofisa hao wakielekea katika gari la polisi jana baada ya kukamatwa |
Kukamatwa kwa maafisa hao kumefuata baada ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa Mhasibu Mkuu katika ofisi hiyo ya waziri mkuu Bw Geoffrey Kazinda jumapili iliyopita kufuatia taarifa ya Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw Pius Bigirimana, kwamba mhasibu huyo alishindwa kusimamia vyema mali za serikali.
Mkurugenzi wa upelelezi nchini Uganda Bi Grace Akullo amethibitisha kukamatwa kwa maafisa hao ambapo licha ya sheria kueleza kuwa mtuhumiwa anatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 baada ya kukamatwa, lakini Bw Kazinda amekwiha kaa kizuizini kwa zaidi ya muda huo

No comments:
Post a Comment