Mafisadi EPA miaka 18 kila mmoja
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam,imewahukumu washitakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kujipatia fedha isivyohalali kutoka kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya nje [EPA]
kwenda jela miaka 18 kila mmoja
Hukumu ambayo ilisomwa na Hakimu Kahyoza na aliitoa kwa kusema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi saba wa upande wa mashtaka mahakama bila kuacha shaka imeona washtakiwa hao wana hatia kwenye makosa sita kati ya saba waliuyoshitakiwa
Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya washitakiwa hao kupatikana na hatia ya makosa sita kati ya saba waliyokuwa wanakabiliwa nayo ikiwemo la kujipatia fedha Sh. bilioni 2.2 za Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje (Epa) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kufuatia kifungo hicho wametimiza jumla ya miaka 18 jela ambapo awali walishahukumiwa kifungo cha miaka mitano ambapo hukumu hiyo itakwenda sambamba na kile cha awali
Hukumu hiyo ya imeainisha kuwa kwa kila kosa watatumikia miaka mitatu jela ambapo wamepatikana na makosa sita limo la kula njama, kughushi nyaraka, kuwasilisha hati bandia na kujipatia Sh. 2,266,049,041.25 kutoka katika Benki hiyo
Kwa mujibu wa Hakimu, washtakiwa hao wataanza kutumikia kiifungo hicho kuanzia jana sambamba na kifungo cha awali.
Awali katika kesi ya msingi, washtakiwa hao walidaiwa kuwa Machi 20 -25 Desemba, mwaka 2005 washitakiwa hao walijipatia hizo wakidai kwamba Kampuni ya B.Graciel ya Ujerumani imehamishiwa deni na Kampuni ya Money Planers & Consultant ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment