FLASH

Friday, July 27, 2012

SHIRIKA LA TCRS NGARA LASISITIZA UWAZI KATIKA UTENDAJI


Viongozi wa vijiji na kata wilayani Ngara Mkoani Kagera, wameshauriwa kufanya kazi kwa uwazi ili kuepusha mgongano baina yao na wananchi wanaowaoongoza

Ushauri huo umetolewa na shirika lisilo la kiserikali la TCRS wilayani Ngara kupitia kwa mwezeshaji wake Bw William Mnyanga alipokuwa akizungumza na wenyeviti wa vijiji, watendaji na madiwani kutoka katika kata zilizo kwenye mradi wa shirika hilo
Bw William Mnyanga akitoa daras kwa Viongozi hao
Amesema kuwa uwazi hasa katika mapato na matumizi unapaswa kupewa kipaumbele na viongozi katika maeneo yao kwa kuwa migogoro mingi baina ya viongozi na wananchi husababishwa na kutokuwepo kwa uwazi


Aidha Bw Mnyanga amesema kuwa kupata taarifa ni haki ya msingi ya kikatiba ambayo kila mwananchi anastahili kuipata kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Katika hatua nyingine diwani wa kata ya Rulenge Bw Hamisi Baliyanga ameishauri halmashauri ya wilaya Ngara kuwekeza katika ufugaji wa samaki ili kuongeza vyanzo vya mapato

Amesema kuwa licha ya kuongeza pato lakini pia ufugaji wa samaki utaboresha afya za wananchi kwa kuwa samaki huongeza protini mwilini
Kulia ni mimi nikiwa na washiriki wengine tukifuatilia kwa makini
Bw Baliyanga amesema vijiji vingi havina vyanzo vya kutosha vya mapato hali inayochelewesha maendeleo ya vijiji husika na halamsahauri kwa ujumla
Mmoja wa washiriki akitafakari jambo.....!!!!!!
Kwa upande wake bw Mnyanga amesema kuwa shirika la TCRS limewawezesha wananchi wa vijiji vya Nterungwe,Chivu na Bukirilo wilayani Ngara ambao wamechimba mabwawa na kufuga samaki na kwamba vijiji vya Nyakiziba, Murukulazo na Munjebwe tayari vimkechimba mabwawa na sasa kinachosubiriwa ni vifaranga vya samaki kwa ajili ya kuwafuga

No comments:

Post a Comment