FLASH

Tuesday, July 31, 2012

TAARIFA YA TANZIA

EVEREADY NKYA WA TCRS NGARA NA KARAGWE AFARIKI

Mratibu wa Mradi katika shirika la TCRS wilaya za Ngara na Karagwe mkoani Kagera Bw Eveready Nkya amefariki usiku wa kuamkia Leo July 31,2012 katika hospitali Teule ya wilaya ya Ngara Murgwanza

Bw Nkya amefariki kutokana na tatizo la kubanwa kifua hali iliyomlazimu kulazwa hospitalini hapo tangu jumapili mchana baada ya hali yake kutokuwa nzuri
Eveready Nkya (Kulia) akiwa na Ayman Sadek Taqawi wa Misri walipokuwa mjini Geneva Uswisi, 2003
Dalili za ugonjwa huo zilimuanza Bw Nkya tangu alhamisi ya tarehe 26 mwezi July ambapo hakuwa amezidiwa hadi kuweza kunipigia simu na kunieleza kuwa hajiskii vizuri na hivyo aliniarifu kuwa asingeweza kuhudhuria katika mafunzo aliyokuwa ayaendeshe kwa wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na madiwani kutoka kata sita zilizo kwenye mradi wa shirika hilo siku ya Ijumaa tarehe 27,July

Hali hiyo ilimlazimu msaidizi wake Bw William Mnyanga kuendesha mafunzo hayo akisaidiwa na wawezeshaji wengine wa shirika hilo na hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kuongea naye kabla ya kupelekwa hospitali

Kifo cha Bw Nkya ni pigo kwa wanaharakati nchini, wapenda haki na watetezi wa wanyonge hasa kuhusu rasilimali na fedha za umma

Mipango ya kuusafirisha mwili wa Marehemu kwenda Moshi kwa Mazishi inafanywa nyumbani kwake TCRS COMPOUND mjini Ngara

Mungu ibariki Familia yake na kuipa moyo wa subra na uvumilivu katika wakati huu mgumu

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU EVEREADY NKYA MAHALI PEMA PEPONI, AMINA

No comments:

Post a Comment