FLASH

Friday, July 20, 2012

WABUNGE WASUSIA KIKAO BAADA YA SPIKA KUGOMA KUJADILIWA KWA AJALI YA MV SKAGIT



Wabunge wa upinzani na baadhi ya wanaotoka Zanzibar Leo wamesusia kikao cha bunge na kutoka nje ya ukumbi wa bunge baada ya Naibu Spika kukataa kujadiliwa kwa ajali ya meli ya Mv Skagit iliyotokea juzi karibu na Bandari ya Zanzibar

Naibu spika Bw Job Ndugai amekataa hoja hiyo akisema kuwa pamoja na uhumimu wa suala hilo, wabunge wahakuiunga mkono hivyo haitajadiliwa

Awali mbunge wa Singida mashariki Bw Tundu Lissu aliomba bunge liahirishe ratiba zake ili wajadili juu ya ajali hiyo ambayo imepelekea vifo vya zaidi ya watu 60 na wengine hawafahamiki waliko hadi sasa

Naibu Spika akishirikiana na mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, uratibu na Bunge Bw William Lukuvi waliungana kupinga jambo hilo lisijadiliwe ndani ya bunge 
Miongoni mwa manusura wakijiokoa
Wakati huo huo Idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli ya Skagit iliyotokea juzi tarehe 18/07/2012 katika eneo la Chumbe wakati ikitokea Dar es salaam kwenda Zanzibar imefikia 63

Hadi jana jioni maiti 63 zilikuwa zimeopolewa huku watu wengine 146 wakiokolewa wakiwa hai na 81 bado hawajulikani walipo licha ya juhudi za uokoaji kuendelea kwa msaada wa ndege ya Umoja wa Ulaya.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya Maisara kuwatambua ndugu zao
Hata hivyo, Msemaji wa Polisi visiwani Zanzibar, Mohamed Mhina, amesema juhudi za uokoaji zinaendelea lakini kuna matumaini kidogo ya kuwapata watu hao wakiwa hai
Rais Jakaya Kikwete na Dr Ali Mohamed Shein wakiwa katika viwanja vya Maisara
Kufuatia ajali hiyo, Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete, alifika katika viwanja vya Maisara ambako wananchi wanaendelea kutambua maiti za ndugu zao

No comments:

Post a Comment