FLASH

Friday, July 20, 2012

WANAWAKE 578 KATI YA LAKI MOJA HUFARIKI WAKATI WA KUJIFUNGUA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema ni jambo lisilokubalika kwa mwanamke kupoteza maisha wakati akijifungua kwa kuwa ujauzito sio ugonjwa

Amesema pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali za kupunguza vifo vya kinamama wakati wa uzazi bado tatizo ni kubwa na zinahitajika juhudi zaidi ili kuondokana na tatizo la vifo wakati wa uzazi

Rais Kikwete amesema hayo jana wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Pathfinder International, Dr. Purnima Mane, Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete akiwa na Dr Mane Ikulu jana
Takwimu za sasa zinaonyesha kuwa kinamama 578 kati ya laki moja hupoteza maisha wakati wa uzazi, idadi ambayo imeshuka kutoka miaka minne iliyopita wakati takwimu zilionyesha kuwa kinamama 790 kati ya laki moja walikuwa wanapoteza maisha wakati wa kujifungua.
Rais Kikwete akiwa na Dr Mane pamoja na ujumbe alioambatana nao Ikulu hapo jana
Aidha Dr Mane amempongeza Rais Kikwete kwa juhudi za kukabiliana na vifo vya kinamama wajawazito wakati wa kujifungua pamoja na uboreshaji wa afya kwa ujumla

No comments:

Post a Comment