FLASH

Friday, July 20, 2012

MKUU WA WILAYA YA NGARA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA SHULE


Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu amemsimamisha kazi mkuu wa shule ya sekondari Kabanga wilayani hapa Bw Enock Ntakisigaye ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za ubadhirifu wa mali ya umma na kutumia vibaya madaraka

Bw Costantine Kanyasu amefanya uamuzi huo jana ambapo amemsimamisha mkuu huyo wa shule kwa muda wa siku 14 kufuatia kikao cha dharura cha bodi ya shule hiyo kilichohudhuriwa na watumishi wa shule na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu wa tatu kulia
Amesema watumishi wa shule hiyo wanamtuhumu Bw Ntakisigaye kwa kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo, kusababisha makundi ya kiutendaji kwa watumishi wa shule hiyo na kutumia lugha ya vitisho

Tuhuma nyingine ni kushindwa kusimamia maagizo ya bodi ya kuwachukulia hatua wanafunzi wasio na nidhamu, na kufuja mali za shule kwa manufaa binafsi ikiwa ni pamoja na usafiri wa shule hiyo

No comments:

Post a Comment