FLASH

Thursday, July 19, 2012


WABUNGE WA RWANDA WAPINGA KUASILI WATOTO
Wabunge wa Rwanda wameitaka serikali kufuatilia habari za watoto wa nchi hiyo ambao huchukuliwa na raia wa kigeni kwa ajili ya kutunzwa 

Wabunge hao wamehoji sera ya nchi hiyo juu ya suala la kuasiliwa kwa watoto wakisema kuwa watoto wanaopelekwa nje ya nchi hiyo wanapoteza uasili wao 
Rais Paul Kagame wa Rwanda
Takwimu za serikali ya Rwanda zinaonyesha kuwa zaidi ya watoto 2060 wa nchi hiyo wamechukuliwa na kupelekwa nje katika kipindi cha kati ya mwaka 2006 na 2009 

Chini ya utaratibu huo watu wanaohitaji watoto wamekuwa wakifuata sheria na kuwachukua watoto hao ambao wengi wamepelekwa Marekani, Ufaransa, Italia na Ubelgiji

No comments:

Post a Comment