FLASH

Thursday, September 6, 2012

MKESHA MBIO ZA MWENGE HAUNA UHUSIANO NA MAAMBUKIZI YA VVU, ASEMA DC NGARA



Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu amevitaka vyama vya siasa kutoa ushirikiano kwa serikali katika mbio za mwenge wa uhuru unaotarajiwa kupokelewa wilayani Ngara kesho ukitokea wilayani Karagwe

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake kuhusu maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru, Bw Kanyasu amesema mbio za mwenge wa uhuru zina malengo maalum ikiwemo kuzindua miradi ya maendeleo pamoja na kusambaza elimu kupitia ujumbe wa mwenge kwa kila mwaka
Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu aliyeshika kidevu
Amesema kuwa miradi inayozinduliwa na mwenge inawanufaisha wananchi wote wa maeneo husika bila kujali itikadi zao za kisiasa hivyo wanasiasa hawapaswi kupotosha malengo ya mwenge huo kwa wananchi

Mwenge wa uhuru utawasili kesho wilayani Ngara kwa kupokelewa katika eneo la Benaco ambapo miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 635 itakaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa wilayani Ngara

Bw Kanyasu Kushoto akiwa na Samwel Sitta

Wakati  huo huo Bw Constantine Kanyasu amesema kuwa mikesha ya mbio za mwenge haina uhusiano wowote na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi


Amesema kuwa maambukizi ya ukimwi huweza kutokea popote kutokana na tabia ya mtu

Aidha Bw Kanyasu ametoa wito kwa wananchi wa maeneo ambayo mwenge huo utapita wajitokeze kwa wingi

No comments:

Post a Comment