BADO ELIMU INAHITAJIKA KUPAMBANA NA UNYANYASAJI WA WENYE ULEMAVU WA NGOZI
Majuzi kamera ya blogu hii ilikuwa sehemu ya kipindi cha Radio Maria kilichorushwa hewani live kutoka Mwanza toka Parokia ya Kirumba, Mada kuu ilikuwa kujadili ni namna gani ya kuwanususru ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi toka kwenye lindi la manyanyaso linalowakabili toka kwa baadhi ya familia hapa nchini. |
Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikisomeka kuwamiongoni mwa nchi ambazo zimefanikiwa kulinda amani na utulivu wa nchi, lakini baada ya kutokea kwa mauaji ya ndugu zetu hawa wenye ulemavu wa ngozi maeneo ya kanda ya ziwa, taswira imebadilika kwa kuchafua uhalisia wa amani ya nchi. |
Ingawa
kwa sasa lile wimbi la mauaji yenye nia ya kuchukuwa viungo vya miili
ya albino limedhibitiwa lakini bado ndugu zetu hawa wanakabiliana na
tatizo jingine la unyanyapaa, suala ambalo limekuwa sugu na kuwaathiri
wengi kulingana na maeneo wanayoishi watu hao. Unyanyapaa umekuwa na viwango vyake na uko kwenye madaraja.. kwani kwa maeneo ya mijini suala la unyanyapaa limedhibitiwa kupitia usambaaji wa elimu itolewayo kupitia radio mbalimbali, majarida, makongamano na mitandao ya kijamii tofauti na ngazi ya wilayani na vijijini ambako mijadala imekuwa michache na upashaji habari hauna nyenzo za kuwafikia wananchi. |
Walemavu
wengi wa ngozi, ngozi zao kushindwa kuhimili mionzi ya jua hivyo
kushambuliwa na maradhi ya kansa ya ngozi na kadhalika, pamoja na kuwa
na uoni hafifu unaowapa shida kujisomea au kupata elimu darasani
wamejikuta wakitengwa na ndugu zao na hata jamii zinazo wazunguka
kutokana na jamii hizo kutopewa elimu ya kutosha inayowawezesha
kuwatambua. Wengi bado wana fikra potofu kwamba kuwa albino ni laana. Elimu bado inahitajika ndugu zangu. |
No comments:
Post a Comment