Mbunge mwanamke wa kuteuliwa kutoka wilaya ya Butaleja nchini Uganda Bi Cerinah Nebanda Arioru, amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini huku kifo chake kikiwa na utata
Kifo cha mbunge huyo mwenye umri wa miaka 24 kimetokea jana jioni katika hospitali ya Mukwaya iliyo karibu na ubalozi wa Marekani nchini Uganda
Bi Cerinah Arioru aliyechaguliwa kuwa mbunge mwaka 2011 |
Mbunge wa Kigulu Kusini Bw Milton Muwuma amesema kuwa kifo cha mbunge huyo kimeibua hofu kwa wabunge nchini humo kutokana na mazingira yake
Imeelezwa kuwa wanaume wawili akiwemo mtu anayedaiwa kuwa mpenzi wake walimfikisha hospitalini hapo mbunge huyo na kumtelekeza kisha kuelekea
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Uganda IGP Kale Kayihura ameagiza kikosi maalum kufanya uchunguzi juu ya kifo hicho na kuhakikisha wanawakamata wanaume hao ambao pia walitelekeza gari la mbunge huyo hospitalini hapo
No comments:
Post a Comment