Mwanamke ambaye alimshitaki mwajiri wake nchini Kenya kwa kumfukuza kazi kinyume cha sheria pamoja na kumbagua kutokana na ulemavu wa viungo ameshinda kesi na kulipwa fidia ya shilingi milioni 13.5
Hakimu Byram Ongaya amemtia hatiani mwajiri wa mpango wa pensheni wa Teleposta kwa kumfukuza kazi kimakosa Bi Beatrice Osir
Bi Osir akiwa nyumbani kwake mjini Nairobi baada ya kushinda kesi hapo jana |
Bi Osir aliyekuwa meneja msaidizi wa mradi huo kabla ya kufukuzwa kazi pia atapewa shilingi laki tano nyingine kutokana na kubaguliwa kwa ulemavu wake
Aidha bodi ya wadhamini ya mpango huo wa Teleposta Pension, imetakiwa kuchagua kati ya kumrejesha kazini Bi Osir au kumlipa kiasi hicho cha fedha na endapo itamrejesha kazini kuanzia Januari mosi mwakani, Bi Osir atafanya kazi mfululizo kwa miaka kumi zaidi
No comments:
Post a Comment