HAPA KAKA NDULANGO UMENENA
Nakumbuka
mwaka 1986 kwa mara ya kwanza nafika Dodoma kuhudhuria mkutano mkuu wa
Chipukizi Taifa nikiwa kama Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Ilala
mkutano uliofanyikia iliyokuwa Shule ya Sekondari Mazengo, ambayo leo
ndio mahali kilipo Chuo kikuu cha Mtakatifu John, wakati huo Mwenyekiti
wa Wilaya ya Temeke akiwa Ndugu Fredy Mwatonoka Mwanjala, Kinondoni
akiwa Athuman Kapunguti na Mkoa alikuwa Ndugu Mohamed Zuberi Mkoto.
aidha nilirudi tena Dodoma mwaka 2006 nikiwa Katibu wa UVCCM wa Wilaya
nikitotea Wilaya ya Ilala pia kama Katibu wa Wilaya na kuondoka Dodoma
nikiwa Katribu wa UVCCM Mkoa kuelekea Iringa mwaka 2007, katika kipindi
nilichoondoka unapozungumzia vyuo Dodoma unazungumzia Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) na Mipango ambavyo havikuwa na hadhi ya Vyuo vikuu
Nambieni leo kuna Vyuo vikuu vingapi Dodoma maana wale wepesi wa kubeza
kwa kutojua tulip[otoka tunawataka mtambue huu ukweli wa Historia ya
Dodoma.
Maana wengine wamekuja Dodoma kwa kuwa tu tayari Serikali ya CCM
chini ya Dr. Jakaya Kikwete imeshawatengenezea Fursa ya elimu ndio
wanaiona Dodoma ya leo. Hivyo sie vijana wa kati tuna wajibu wa kuwajuza
wale wasioelewa tulipotoka na hapa tulipo maana wengine wamekuja na
wamekuta tayari kile kijiji cha Chimwaga maghorofa yametengeneza mji
waulize wenyeji wawajuze ndio maana naendelea kusisitiza kuwa wasione
vyaelewa wajue vimeundwa na waundaji ndio CCM chini Mhe. Dr. J.M.
Kikwete.
Kwa mantiki hiyo miaka saba iliyopita Dodoma haikuwa kama
unavyoiona leo . VIVA CCM VIVA.... NA VIVA KIKWETE VIVAAAAAAAH.
Kwa hisani ya www.facebook.com/Josephat Hamidu Ndulango
No comments:
Post a Comment